LIFESTYLE
SMS 10 za kubembeleza na kuchochea mahaba
Natamani ningekuwa chozi jichoni mwako ambapo
ningetelemka
na kuishia midomoni mwako,
lakini kamwe sitamani uwe chozi
jichoni mwangu nitakupoteza kila muda niliapo.
******
Kumbuka kuwa wewe ni wangu
Kitulizo cha moyo wangu
Kwenye shida na raha
Wewe ni sehemu ya maisha yangu milele
******
Bongo zenye fikra kali huwa na mawazo,
suluhu na sababu;
ubongo wa kisayansi huwa na kanuni,
nadharia na takwimu;
wangu una wewe tu!
********
Anayekupenda ni mimi, watakaokutamani ni wengi,
Tafuta dunia nzima penzi langu la kweli huwezi kulipata,
penzi langu
kwako ni nuru daima halizimiki.
*****
Nilikuwa nikifiria kwamba ndoto haziwezi kuwa kweli,
lakini nilibadili mawazo yangu pale tu nilipokuona wewe
******
Hakika sikutaraji kulikosa lako penzi, wataka kuniacha
kuniacha ningali nakuhitaji, mpenzi tambua nahitaji yako
hifadhi na niko radhi kukupeleka hadi kwa wangu wazazi,
amini kwenda kwa mwingine sihitaji. Nakupenda
******
Hakika wewe ndiye wangu mahabuba
unayejua kunipa huba,
napenda unavyoniganda mithili ya ruba,
nahahidi kukupa
mahaba yanayozidi shaba. Nakupenda.
******
Pokea sms yangu iliyojaa utamu,
nimeipamba kwa maneno laini yenye ladha adimu,
utamu wake ni kama apple haufanani na ndimu,
nimeituma kwako sms hii ikuletee salamu
“UHALI GANI MPENZI?”
