Njia 6 za kumjua msichana ambaye hakupendi
Njia 6 za kumjua msichana ambaye hakupendi
1. Anakataa kukupa namba mara ya kwanza
Ikiwa msichana hataki kukupa namba yake ya simu
Unapomuomba mara ya kwanza, jua ya kwamba hakutaki.
Ikiwa atakupa, itachukua muda kufanya hivyo,
jua kuwa hataki mambo yako, hivyo ni bora kukoma
mapema kwa sababu mtasumbuana bure tu.
2. Amekupa namba isiyo yake
Msichana akifanya hivi huhitaji kungoja sana kujua
kuwa hapendezwi nawe. Kushinda ukimfuata
itakuumiza bure tu kwani simu zako zitakuwa
zikichuliwa na mtu mwingine.
Huenda akalaumu mfumo mbaya ya mawasiliano.
3. Hapokei simu unapompigia
Unangoja nini kujua hakutaki? Ikiwa msichana
atachukua simu mara moja unapopiga, jua ya kuwa
anakupenda na ni ishara kuwa mtakuwa marafiki.
Lakini akichukua muda kujibu, kimbia.
4. Hakutembelei
Ikiwa hatembei kwako, basi ni ishara kwamba
hataki kukuona. Hakuna haja ya kumfuatafuata.
5. Ukisikia marafiki wake wakicheka unapompigia simu
Ikiwa atafanya hivyo, hiyo ni tahadhari, huenda
anakudharau. Utangoja mpaka akuvunje moyo?
Endelea na maisha yake, utapata mwingine anayekupenda.
6. Anapotumia pesa zako ovyo ovyo “Baadhi ya
wanawake sio wema”.
Licha ya kuamua kutokuwa na uhusiano wowote nao,
wanapenda tu kutumia wanaume vibaya kwa
kuwasaidia kuharibu pesa zao walizofanyia kazi kwa bidii.
Ikiwa hakupendi, ataandamana na marafiki wake
wote unapomualika na kukufanya kutumia pesa
zaidi ya ulivyokuwa umepanga.
